Tanzania yaipa kongole GEF kwa kufikia malengo ya ukusanyaji fedha

Aug, 26 2023

Tanzania imepongeza utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Mazingira wa Duniani (GEF) muhula wa saba zikiwemo kufikiwa kwa malengo ya ukusanyaji wa fedha kutoka kwa nchi na wadau wanaouchangia.

Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga jana wakati akichangia hoja katika Mkutano Mkuu wa Saba wa GEF uliofanyika Vancouver, Canada.

Pamoja na michango hiyo ya fedha Tanzania imesisitiza umuhimu wa kuwajengea uwezo wataalam hususan katika kuandaa maandiko ya miradi kwa kuzingatia sera na taratibu za GEF, utakaowezesha uandaaji wa maandiko ya miradi kwa wakati na kuendana na vipaumbele vya nchi husika.

Aidha, Tanzania imeunga mkono mapitio ya muundo na taratibu za uendeshaji wa Mfuko huo yaliyopendekezwa na Baraza la GEF yakilenga kuongeza ufanisi, uwajibikaji na uwazi wa taratibu za uendeshaji wa Mfuko huo.

Settings