Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Tanzania kuneemeka kupitia Uchumi wa Buluu

Apr, 15 2026

Tanzania inatarajia kunufaika kikamilifu na fursa za Uchumi wa Buluu na kuchangia kwa kiwango kikubwa katika pato la taifa, ajira na ustawi wa wananchi.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi wakati akifungua kikao cha Makatibu Wakuu wa Sekta zenye mnasaba na Uchumi wa Buluu uliofanyika jijini Dodoma leo, Aprili 15, 2026.

Amesema kuwa Mpango wa miaka mitano wa Matumizi ya Maeneo ya Maji (MSP) ni mchakato wakimkakati utakaowezesha Taifa kupanga matumizi ya maeneo ya maji kwa kuzingatia mahitaji ya kiuchumi, kijamii na kimazingira.

Aidha, Dkt. Muyungi alieleza kuwa Mpango huo utasaidia kupunguza migongano ya matumizi ya rasilimali za maji, kuongeza uhakika wa uwekezaji na kuhakikisha uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za maji.

Aliongeza kuwa Mpango kazi wa utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu

kwa mwaka 2026/27, umeandaliwa kwa lengo la kurahisisha uratibu na utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu nchini ili kufikia malengo mahsusi yaliyoainishwa katika Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu ya mwaka 2024 na Mkakati wake wa utekelezaji.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Baraka Luvanda alisema kikao hicho ni muhimu kwa ajili ya kupitia hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu (Julai-Desemba 2025).

Balozi Luvanda alieleza kuwa washiriki wanapata nafasi ya kujadili mafanikio, changamoto pamoja na kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha utekelezaji wake.

“Kikao hiki kitatupatia fursa ya kupitia na kuridhia Mpango Kazi wa utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu kwa mwaka wa fedha 2026/27, ili kuhakikisha kuwa sekta zote husika zinaendelea kushirikiana kwa ufanisi katika kukuza mchango wa Uchumi wa Buluu katika maendeleo ya taifa letu,” alisema.

Halikadhalika, Balozi Luvanda alisema kupitia kikao hicho washiriki wanajadili Mpango Kazi wa Uandaaji wa Mpango wa Matumizi Endelevu ya Maeneo ya Maji (Marine Spatial Planning -MSP) kwa kipindi cha mwaka 2025-2030, ambao ni nyenzo muhimu katika kupanga na kusimamia matumizi endelevu ya rasilimali za bahari na maji baridi kwa ujumla, kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Ikumbukwe kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imepewa majukumu la kuratibu utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu Tanzania Bara, ikiwemo kuratibu vikao vya Kamati ya Makatibu Wakuu na Kamati ya Mawaziri wa sekta zenye mnasaba na masuala ya Uchumi wa Buluu.

Pia, ina jukumu la kuhakikisha inaratibu, inafuatilia na kufanya tathmini ya utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu nchini, ikiwemo shughuli zinazotekelezwa na sekta zenye mnasaba na masuala ya Uchumi wa

Buluu.

Habari

Settings