Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Tanzania, Djibouti kuimarisha ushirikiano biashara ya kaboni

Aug, 25 2026

Serikali za Tanzania na Djibouti zimeimarisha ushirikiano katika masuala mbalimbali ya kimkakati ikiwemo biashara ya kaboni na ufadhili wa miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yamejiri wakati wa ziara ya Ujumbe wa Tanzania ya kubadilishana uzoefu wa usimamizi wa biashara ya kaboni, upatikanaji wa fedha za mabadiliko ya tabianchi na kutumia sekta za kimkakati za uchumi za kuchochea maendeleo endelevu, iliyofanyika nchini Djibouti Agosti 23 hadi 25, 2026.

Katika mazungumzo kati ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Djibouti akiwemo Waziri Mkuu Mhe. Abdoulkader Kamil Mohamed walizungumzia pia fursa za kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa katika sekta za bandari, usafiri wa baharini na anga

Akizungumzia ziara hiyo, Dkt. Muyungi alieleza kuwa Tanzania tayari imepiga hatua kubwa katika kujenga soko la kaboni na hatua inayofuata ni kuhakikisha fursa hiyo inatafsiriwa kuwa chanzo endelevu cha mapato, uwekezaji, ajira, uhamishaji wa teknolojia na manufaa ya moja kwa moja kwa jamii zinazohifadhi rasilimali za asili.

Alisema hadi kufikia Julai 2026, Tanzania ilikuwa na miradi 117 ya biashara ya kaboni iliyosajiliwa huku miradi minne mikubwa iliyoidhinishwa Agosti 2026 inahusisha takribani tani milioni 4.2 za viwango vya kaboni vilivyohakikiwa, vyenye thamani inayokadiriwa kuzidi Dola za Marekani milioni 52.1, sawa na takribani Shilingi bilioni 135.5.

Alieleza kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni (NCMC) itaendelea kuratibu hatua za ufuatiliaji wa maeneo yaliyojadiliwa ili kuhakikisha mafunzo yaliyopatikana yanachangia katika kujenga uchumi wa kaboni wenye uadilifu, ushindani na manufaa kwa Taifa, sambamba na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo.

Dkt. Muyungi aliongeza kuwa Tanzania iliwasilisha rasmi taarifa ya awali ya Ibara ya 6.2 ya Makubaliano ya Paris kwa Sekretariat ya Mkataba wa UNFCCC Mei 20, 2026, hatua inayoiweka nchi katika nafasi nzuri ya kushiriki katika mifumo ya kimataifa ya biashara ya kaboni.

“Jambo muhimu katika ziara hiyo lilikuwa kujifunza kuhusu Sovereign Carbon Initiative ya Djibouti, hususan mfumo unaounganisha shughuli za wazalishaji wakubwa wa hewa ukaa na ukusanyaji wa mapato ya kaboni, mfumo wa usajili na uelekezaji wa fedha hizo katika miradi ya kitaifa ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi,” alisema.

Aidha, Dkt. Muyungi aliongeza kuwa uzoefu huo una umuhimu kwa Tanzania katika kuendelea kujenga mfumo wa biashara ya kaboni wenye uadilifu, uwazi, manufaa kwa taifa na unaolinda maslahi ya wananchi.

Katika sekta ya usafiri wa baharini, ujumbe ulipata fursa ya kujifunza namna Djibouti inavyotumia nafasi yake kama kitovu muhimu cha bandari na biashara katika Pembe ya Afrika kuunganisha shughuli za kiuchumi na kupatavl fedha za mabadiliko ya tabianchi.

Pande hizo zilijadili maeneo yanayoweza kuendelezwa, ikiwemo biashara ya kaboni katika shughuli za baharini, viwango vya bandari za kijani, mifumo ya kidijitali ya upimaji na utoaji taarifa, uwekezaji katika miundombinu ya bandari inayofadhiliwa kupitia mapato ya kaboni na uwezekano wa kuendeleza njia za usafiri wa baharini zisizozalisha hewa ukaa kwa kiwango kikubwa (green shipping corridors).

Ziara hiyo imeweka msingi muhimu wa kuendeleza ushirikiano wa kitaalam na kitaasisi kati ya Tanzania na Djibouti, ikiwemo kubadilishana utaalam na uzoefu katika utawala wa masoko ya kaboni, mifumo ya kidijitali, ufadhili wa tabianchi, usimamizi wa mapato ya kaboni na matumizi ya sekta za kimkakati kuongeza thamani ya rasilimali za kaboni.

Viongozi wengine wa Djobouti waliofanya mazungumzo na Ujumbe wa Tanzania ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Abdoulkader Houssein Omar, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Bw. Mohamed Abdillahi Waïs pamoja na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Bandari na Maeneo Huru ya Djibouti (Djibouti Ports and Free Zones Authority) Bw. Aboubaker Omar Hadi.

Kwa upande wa Tanzania Dkt. Muyungi aliambatana na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya NCMC Mhe. Khamis Hamza Khamis Afisa Mtendaji Mkuu wa NCMC Bi. Kathryn Kigaraba pamoja na wataalam kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na NCMC.

Habari

Settings