Serikali kutenga bajeti kukamilisha ujenzi wa kingo za Mto Msuka

May, 09 2024

Naibu Waziri Khamis Hamza Khamis akijibu maswali bungeni leo Mei 09, 2024 amesema Serikali kutenga bajeti kukamilisha ujenzi wa kingo za Mto Msuka

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Ilemela Mhe.Angeline Mabula lini ujenzi huo utakamilika.

Mhe. Khamis amesema kuwa ujenzi unaendelea ambapo hadi sasa daraja na kingo zake zenye urefu wa takribani mita 500 umekamilika.

Halikadhalika, amesema Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kupitia mradi wa Tanzania Cities Transforming Infrastructure and Competitiveness (TACTIC) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia imeomba shilingi bilioni 6.75 kwa ajili ya ujenzi wa barabara pamoja na kukamilisha ujenzi wa kingo za mto Msuka ambapo ujenzi wake utaendelea baada ya fedha zilizoombwa kupatikana.

Kwa upande mwingine ameahidi kufanya ziara wilayani humo ya kukagua athari zilizojitokeza kutokana na maji ya kufurika na kuharibu miundombinu na kuona namna gani Serikali itakavyoshughulikia ilinkuwasaidia wananchi.

Settings