Sekretarieti ya Kamati ya Pamoja yajadili masuala ya Muungano

Feb, 21 2025

Sekretarieti ya Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imekutana kujadili masuala ya Muungano jijini Dar es Salaam leo tarehe 21 Februari 2025.

Kikao hicho kimeongozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja pamoja na Mwenyekiti Mwenza ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Bw. Islam Seif Salum.

Aidha, kikao hicho pia kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu (SMZ) Bw. Saleh Juma Mussa, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (SMZ) Bi. Mansura Mosi Kassim na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi.

Wengine ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria (SJMT) Bi. Angela Anatory, Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi, Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Juma Mohamed Salum ambaye pia ni Katibu wa kikao na Mkurugenzi wa Uratibu na Shughuli za Serikali Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Bi. Siajabu Suleiman Pandu (Katibu Mwenza) pamoja na wataalamu kutoka SJMT na SMZ.

Hivyo, Kikao cha Sekretarieti ya Kamati ya Pamoja ya SJMT na SMZ hufanyika kwa mzunguko katika kila upande wa Muungano kujadili masuala ya Muungano.

Settings