Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024, Kampeni ya Soma na Mti yatekelezwa kwa vitendo

Apr, 06 2024

Kampeni ya ‘Soma na Mti’ imeendelea kutekelezwa kwa vitendo wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 mkoani Kilimanjaro ambapo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Pumuani wamepanda miti 625 eneo la shule hiyo.

Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wengine wa shule hiyo Aprili 6,2024, Christian Msoffe amesema upandaji wa miti katika shule yao imesaidia kuweka mazingira ya kupendeza na mazuri.

“Utekelezaji wa ujumbe mkuu wa Mwenge 2024 kwa upande wa utunzaji wa mazingira, shule yetu tayari imepanda miti 265 ikiwa ni jitihada ya kuhakikisha shule yetu inapendeza na tunakuwa na mazingira mazuri ya kujifunzia,” amesema Msoffe.

Kampeni ya ‘Soma na Mti’ ilizinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe Dkt. Selemani Jafo katika Shule ya Sekondari Dodoma Januari 20,2022 jijini Dodoma.

Kampeni ya ‘Soma na Mti’ ni Kampeni ya upandaji wa miti kwa wanafunzi wa shule na vyuo ikiwa na lengo la kuwafanya wanafunzi waone zoezi la upandaji miti ni sehemu ya maisha yao ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Waziri Jafo wakati anazindua kampeni hiyo alisema kampeni hii itasaidia kila mwanafunzi ajivunie mti wake alioupanda na kuona fahari kubwa na kujali mazingira na kuijali nchi.

Settings