Katibu Mkuu Maganga afanya mazungumzo na Mtaalamu Elekezi UNEP

Mar, 18 2024

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akiwa katika picha ya pamoja na Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bioanuai (SLR), Dkt. Damas Mapunda (kulia) na Mtaalamu Elekezi kutoka Shirika la Usimamizi wa Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Bw. Warren Olding mara baada ya mazungumzo walipomtembea ofisini kwake jijini Dodoma leo Machi 18,2024 kwa lengo la kutoa Tathimini ya Kati ya utekelezwaji wa Mradi wa SLR.

Mradi wa SLR unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2021 hadi 2025 ambapo jumla ya Mikoa mitano, Halmashauri saba Kata 18 na vijiji 54 vinanufaika na mradi huo.

Halmashauri zinazonufaika na mradi huo ni Halmashauri ya Iringa Vijijini (Iringa), Wilaya ya Mbeya na Mbarali (Mbeya), Halmashauri za Sumbawanga vijijini (Rukwa) pamoja na Halmashauri za Wilaya za Tanganyika na Mpimbwe (Katavi).

Mradi wa SLR ulianzishwa mahsusi na serikali ikiwa ni juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi na shughuli za kibinadamu zisizo rafiki na mazingira ikiwemo ukataji miti, uchomaji mkaa na uharibifu wa vyanzo vya maji ambavyo vimekuwa tishio kwa uhai wa binadamu na viumbe hai.

Mradi wa SLR unafadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) kupitia Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na kusimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais ambapo kiasi cha Bilioni 25.8 kimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

Settings