Katibu Mkuu Luhemeja afunga Jukwaa la Kamati ya Kudumu ya Fedha

Sep, 04 2024

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mha. Cyprian Luhemeja akifunga Jukwaa la Mwaka 2024 la Kamati ya Kudumu ya Masuala ya Fedha chini ya Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi lililofanyika kwa siku mbili kuanzia Septemba 2, 2024 na kufungwa leo Septemba 3, 2024 mkoani Arusha katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

Kumalizika kwa Jukwaa hilo, kesho Septemba 3, 2024 unaanza Mkutano wa 35 wa Kamati ya Kudumu ya Masuala ya Fedha chini ya Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika katika ukumbi huo kwa siku tatu na kufungwa Septemba 6,2024.

Mha. Luhemeja aliwashukuru kwa mara nyingine Wajumbe wa Mkutano kwa kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano, huku akieleza suala la Utunzaji na Uhifadhi wa Mazingira ni suala ambalo kila mmoja anapaswa kujitoa ili kuyalinda.

Ikumbukwe Septemba 2,2024 Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango alifungua Mkutano wa 35 wa Kamati ya Kudumu ya Fedha ya Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC) ambao unajumuiya Jukwaa hilo pamoja na Mkutano huo.

Settings