Kamati ya Usimamizi Mradi wa EMA yajadili Taarifa ya Utekelezaji

Aug, 02 2023

Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa Kuimarisha Uwezo wa Kitaasisi wa Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMA) imekutana kwa ajili ya kupitia taarifa za utekelezaji wa mradi huo katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma Agosti 15, 2022.

Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Ignas Chuwa ameongoza kikao hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga.

Bw. Chuwa ameongoza wajumbe katika kuipitia taarifa ya utekelezaji wa mradi kwa mwaka wa fedha 2022/23 pamoja na bajeti ya 2023/24 ambapo amewahimiza kuusimamia vyema mradi katika utekelezaji wa sheria ya usimamizi wa mazingira.

Pia wajumbe wamepata nafasi ya kuipitia taarifa ya mpango wa matumizi kwa mwaka wa fedha ulioanza Julai 2023 na kutarajiwa na kukamilika Juni 2024 kama ulivyowasilishwa na Mratibu wa Mradi Bw. Richard Masesa.

Mradi wa EMA unaofadhiliwa na Serikali ya Sweden na kuzinduliwa Aprili 12, 2023, unatarajiwa kuboresha uratibu wa usimamizi wa mazingira nchini unaokusudia kushughulikia changamoto kuu za mazingira.

Settings