Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Dkt. Dugange ateta na Waziri Hamza Zanzibar

Nov, 30 -0001

Naibu Waziri Ofisi Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange amefanya mazungumzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi ) Mhe.Hamza Hassan Juma wakati wa ziara ya kikazi leo Februari 16, 2026 Zanzibar.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa Serikali hizo mbili katika kulinda Muungano.

Naibu Waziri Dkt. Dugange alipongeza kazi kubwa ya maendeleo inayofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) chini ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Alisema kuwa kupitia maendeleo hayo yanaimarisha uchumi wa Zanzibar na ndio matunda ya Muungano.

Kwa upande wake Waziri Hamza alitoa rai kwa watendaji kutangaza zaidi fursa za zinazopatikana katika Muungano badala ya changamoto.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na viongozi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Habari

Settings