Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Serikali yaendelea kutatua hoja za Muungano

May, 22 2026

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zimeendelea kuzipatia ufumbuzi hoja za Muungano baada ya Kamati ya Pamoja ya kutatua hoja 23 kati ya 25 zilizokuwa zikishughulikiwa tangu mwaka 2006.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa wakati akitoa taarifa bungeni baada ya kuibuka hoja ya Mbunge kuhusu bidhaa zinazozalishwa Zanzibar kupata kizuizi cha kuuzwa Tanzania Bara.

Akiendelea kutoa taarifa, alisema katika kikao cha Kamati ya Pamoja ya SJMT na SMZ kilichoketi Aprili 25, 2026 Zanzibar chini ya Mwenyekiti Makamu wa Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Hoja ya Uingizaji wa Sukari kutoka Zanzibar katika Soko la Tanzania Bara ilitatuliwa na kuondolewa kwenye orodha ya Hoja za Muungano.

“Tunao utaraibu tuliojiwekea kama nchi wa kushughulikia masuala ya hoja za Muungano na tangu mwaka 2006 tulipitisha utaratibu wa kuwa na Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kushughulikia hoja zote zinazojitokeza,” alisema.

Alisisitiza kuwa utaratibu huo umetumika pia kutatua changamoto nyingine za biashara ikiwemo bidhaa za maziwa, huku akisisitiza kuwa mfumo wa kutatua hoja za Muungano ni wa ndani na unaokubalika kwa pande zote mbili za Muungano.

Habari

Settings