Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Serikali kuhakikisha wananchi wanapata elimu biashara ya kaboni

Apr, 17 2026

Serikali imesema itaendelea kuimarisha juhudi za kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa kutosha na kushiriki kikamilifu katika biashara ya kaboni ili kunufaika kiuchumi huku wakichangia uhifadhi wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Josephine Kapoma aliyetaka kujua Serikali ina mkakati gani wa kufikisha elimu kwa wananchi kuhusu biashara ya kaboni.

Akijibu swali hilo bungeni jijini Dodoma leo Aprili 17, 2026, Mhe. Kwagilwa alisema Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais na Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni (NCMC) zimeweka mikakati mbalimbali ya kufikisha elimu kwa wananchi.

Alitaja mikakati hiyo kuwa ni kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu dhana, faida na fursa zilizopo katika biashara hiyo kupitia vyombo vya habari na kutoa mafunzo kwa viongozi wa ngazi za mikoa, halmashauri na vijiji ili waweze kuwa mabalozi wa elimu kwa jamii zao kuhusu utekelezaji wa miradi ya kaboni na manufaa yake.

“Tangu kupitishwa kwa Kanuni na Mwongozo wa Biashara ya Kaboni tumetoa elimu kwa viongozi mbalimbali pamoja na kushirikiana na wadau wa maendeleo, asasi za kiraia na sekta binafsi katika kutoa elimu na kujenga uwezo kwa jamii kuhusu namna ya kuanzisha na kunufaika na miradi ya kaboni,” alisema Mhe. Kwagilwa.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kwagilwa alisema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinashirikiana katika kutekeleza miradi ya mazingira na kunufaisha wananchi wa pande zote mbili za Muungano.

Alisema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Amani Mhe. Abdul Yussuf Maalim aliyetaka kufahamu Zanzibar inanufaika vipi na biashara ya kaboni.

Akiendelea kujibu swali hilo, Mhe. Kwagilwa alisema pamoja na kushirikiana katika biashara ya kaboni pia Serikali zote mbili zinashirikiana katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Ikumbukwe kuwa biashara ya kaboni ni mfumo wa kifedha unaoruhusu nchi, taasisi au miradi kupunguza uzalishaji wa gesi joto na kupata faida kwa kuuza au kubadilishana hati za kaboni ambazo hutolewa unapofanikiwa kupunguza au kufyonza hewa ya kaboni.

Habari

Settings