Naibu Waziri Khamis: Fedha za Mfuko wa Jimbo zimeendelea kuleta tija

Apr, 15 2024

Fedha za Mfuko wa Jimbo zimeendelea kuleta tija na matokeo chanya katika kuimarisha na kukuza uchumi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati ameriarifu Bunge wakati akijibu swali la Mbunge wa Wingwi Mhe. Omar Issa Kombo aliyetaka kujua lini Serikali itafanyia kazi changamoto ya Kodi na Tozo kwenye Fedha za Mfuko wa Jimbo kwa upande wa Zanzibar.

Akiendelea kujibu swali hilo Mhe. Khamis amesema kodi na tozo hutozwa kwa mujibu wa Sheria pindi bidhaa au huduma zinapotolewa au kununuliwa.

Amesema bidhaa na huduma zinazotolewa hukatwa kodi ya zuio la kodi (With Holding Tax) kwa kuzingatia Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura ya 332 chini ya kifungu cha 83 (1) (c) kwa malipo ya ada ya kwa huduma kwa ajili ya utoaji wa huduma ya kitaalamu na kifungu (83 A) malipo kwa bidhaa zinazotolewa na mkazi wa uendeshaji biashara.

Halikadhalika, Naibu Waziri amefafanua kuwa kodi hutozwa kwa kuzingatia Sheria ya Manunuzi inayotumika Zanzibar inayojulikana kama sheria zinazotolewa na mkazi wakati wa undeleshaji biashara.

“Mheshimiwa Naibu Spika makato ya fedha yapo kisheria na yanakatwa kodi kwa mujibu wa sheria na ilielekeza na wakurugenzi wa mabaraza ya miji, manispaa wanajua fedha lazima zikatwe kodi,“ amesisitiza Mhe. Khamis.

Aidha, ameongeza kuwa Serikali tayari ilishakaa kikao na wabunge, wenyeviti wa halamshauri wa mabaraza ya miji na manispaa pamoja na taasisi za kukusanya kodi na na wabunge maded na webnyeviti na taasisi za kukusanya kodi Zanzibar na kuwaelimisha wabunge

Settings