Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Mhe. Hemed: Serikali ya Awamu ya Sita kuimarisha usimamizi wa mazingira

May, 29 2026

Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha usimamizi wa mazingira ikiwemo kuboresha sera na sheria za udhibiti wa mazingira nchi.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi. Dkt. Emmanuel Nchimbi katika Ufunguzi wa Maadhimisho ya Miaka 40 ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) uliofanyika katika Ukumbi wa Kiimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Amesema katika kuhakikisha mazingira bora na salama kwa wananchi Serikali inaendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi, na kuimarisha utendaji kazi wa NEMC kwa kuanzisha mchakato utakaoibadilisha kuwa Mamlaka kamili ya Mazingira.

Mhe. Hemed amefahamisha kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali katika kukabiliana na athari za matumizi ya nishati isiyo safi kwa kuendeleza mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia wenye lengo la kuhakikisha asilimia 80% ya Watanzania wanatumia nishati safi ifikapo mwaka 2034, hatua itakayolinda afya, mazingira, na kuboresha maisha ya wananchi.

Aidha, Mhe. Hemed amesisitiza kuwa Serikali inaendelea kuimarisha mipango ya Kitaifa ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, ikiwemo utekelezaji wa mpango wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi ili kuongeza uwezo wa Taifa katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika sekta za maji, kilimo, afya, nishati na miundombinu.

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa zanzibar amesema ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira, Serikali inatekeleza programu na kampeni mahsusi ya ulinzi wa mazingira kwa kupanda miti na kurejesha uoto wa asili ambapo kampeni hio ya Kitaifa iliyolenga upandaji wa miti milioni moja na nusu (1,500,000) kwa kila Halmashauri ili kuongeza wigo wa misitu, kulinda vyanzo vya maji, kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na kurejesha ardhi iliyoharibiwa.

Hata hivyo amesema Serikali imeweka msisitizo katika ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa ili kushughulikia changamoto za mazingira kwa kushirikiana na nchi jirani na Taasisi za Kikanda katika usimamizi wa rasilimali za pamoja, kulinda mifumo ikolojia, na kutekeleza mikataba ya kimataifa ya mazingira, ili kuhakikisha uendelevu wa rasilimali hizi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Mhe. Hemed amesisitiza kuwa ili kufanikiwa katika kupunguza na hatimaye kukomesha kabisa uharibifu wa mazingira ni lazima kutafsiri maneno kwa vitendo katika usimamizi wa mazingira na kuimarisha ushirikiano wa dhati kati ya Serikali, AZISE, Sekta Binafsi na wananchi kwa ujumla na kuweka nguvu za pamoja ili kujenga msingi imara wa ulinzi wa mazingira , kukuza uchumi, na kuhakikisha ustawi wa vizazi vya sasa vijavyo kwa kudhibiti uharibifu wowote wa mazingira.

Nae waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema NEMC imekuwa ni Taasisi muhimu katika kusimamia utekelezaji wa sera, sheria na mifumo ya mazingira kwa lengo la kuhakikisha maendeleo ya Taifa yanaenda sambamba na hifadhi ya mazingira na matumizi endelevu.

Amsema Wizara imejipanga kutatua changamoto zote zinazoikabili Taasisi ya NEMC na kusema kuwa miaka 40 ijayo miji yote itakuwa safi na taka zitatumika kama ni fursa ya kiuchumi.

Mhandisi Masauni amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia pamoja na na kuwa na mazingira safi na salama kwa wananchi wote.

Aidha Mhandisi Masauni amesema dhamira ya wizara ni kuwenda sambamba na malengo ya dira ya marndelelo ya 2050 ambayo imeweka suala la uhifadhi wa mazingira na ustahamilivu wa mabadiliko ya tabia nchi kuwa ni miongoni mwa malengo matatu makuu katika kukuza uchumi wan chi.

Mapema Mtendaji Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Semesi amesema kuwa NEMC inaendelea kutoa elimu juu ya uhifadhi wa mazingira na uhamisishaji wa matumizi mazuri ya nishati safi na salama kwa wananchi wote.

Amesema maadhimisho ya miaka 40 NEMC imeanzisha kampeni juu ya upandaji wa miti kwa halmashauri zote nchini ambapo malengo zaidi ni kupanda miti katika Taasisi za Serikali pamoja na shule za msingi ili kuwajenga wanafunzi kuwa na tabia ya kulinda mazingira.

Aidha Dkt. Immaculate amsema kuwa NEMC imejipanga kuendelelea kuboresha mifumo ya utoaji wa huduma kwa mananchi na wawekezaji kwa kuimarisha matumizi ya teknologia na mifumo katika usimamizi, ufuatiliaji wa utoaji wa vibali na ukusanyaji wa taarifa sambamba na utoaji wa elimu kwa umma juu ya masuala ya mazingira.

Habari

Settings