Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Mhandisi Masauni awasilisha bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwenye Kamati ya Bunge

Mar, 26 2026

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Hamad Yussuf Masauni amewasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2025/26 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Bungeni Dodoma Machi 26,2026.

Mhe. Masauni amesema pamoja na mambo mengine ambayo ofisi inatarajia kuyatekeleza katika mwaka wa fedha ujao hasa eneo la Uchumi wa Buluu ni pamoja na Kuratibu utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu (2024) na Mkakati wake wa Utekelezaji.

Pia kuwajengea uwezo Wataalamu katika masuala ya Uchumi wa Buluu na Kuratibu maandalizi ya Mpango wa Matumizi ya maeneo ya Maji (Marine Spatial Plan – MSP).

Katika masuala ya Muungano Mhe. Masauni amesema Ofisi itaendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ikiwa pamoja na Kuratibu vikao vya ushirikiano baina ya Wizara, Idara na Taasisi za Muungano na Zisizo za Muungano za SJMT na SMZ na kufanya Tathmini ya Vikao vya Ushirikiano.

Pia Ofisi itaendelea kukusanya Nyaraka, na Mikusanyo ya Masuala ya Muungano kwa ajili ya MAKAVAZI ya Muungano pamoja na kuanza hatua za awali za ujenzi wa Vituo vya Kumbukumbu na Nyaraka za Muungano (MAKAVAZI) Dodoma kwa Tanzania Bara na Mkoa wa Mjini Magharibi kwa Zanzibar;

Habari

Settings