Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Masauni akichukulia hatua kiwanda kilichochafua mazingira

Jun, 28 2026

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesitisha kwa muda shughuli za uzalishaji za Kiwanda cha African Steel Group Com. Ltd kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani baada ya kubaini ukiukwaji wa sheria ya usimamizi wa mazingira.

Mhe. Masauni amesema moja ya sababu iliyopelekea kusitiza uzalishaji wa kiwanda hicho kwa muda ni pamoja na uchafuzi wa hewa kutokana na moshi mkubwa unaoweza kuhatarisha afya za wafanyakazi na wananchi wanaoishi jirani na kiwanda.

Pia amesema kiwanda hicho kinalalamikiwa kutiririsha maji taka kwenye mazingira, utupaji taka ovyo, na kukosekana kwa eneo la kuhifadhia chuma chakavu na kupelekea uchafuzi wa ardhi.

Mhe. Masauni ameyasema hayo Juni 27, 2026 akiwa kwenye ziara wilayani Bagamoyo mkoani Pwani alipofanya ukaguzi katika viwanda vitatu akieleza malalamiko kutoka kwa wananchi yalikuwa mengi licha ya kupewa maelekezo mara kadhaa lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.

Ameongeza kuwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kilifanya ukaguzi mara nne kwenye kiwanda hicho na kuwapa maelekezo ya kuboresha, licha ya kuitwa na kusikilizwa changamoto zao lakini hayakufanyiwa kazi.

“Lengo la ziara hiyo ni kuangalia namna uzingatiaji wa sheria ya mazingira inavyofuatwa kwenye viwanda baada ya kugundua kuna viwanda havitekelezi licha ya kuelekezwa na wataaalamu wetu kutoka NEMC”

Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anafanya jitihada kubwa katika kuhamasisha uwekezaji wa viwanda nchini na kweli uwekezaji huo umekuwa ukileta tija ikiwemo kutengeneza ajira na kusaidia kwenye uchumi wa nchi katika makusanyo ya kodi.

“Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na taasisi zake itakuwa ya mwisho kukwaza jitihada hizo za serikali na pia tutakuwa wa mwisho kuacha sheria za nchi yetu ambazo zinakwenda kuokoa uhai wa wananchi wetu zisitekelezwe.”
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi amesema baraza hilo litaendelea kusimamia sheria za mazingira ili kuhakikisha viwanda vinafanya kazi kwa uwajibikaji na kupunguza uchafuzi wa mazingira.

Habari

Settings