Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Shirikisho la Baraza la Maaskofu Katoliki Afrika ya Kati (ACEAC) linalojumuisha nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na Rwanda, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhashamu Askofu José Moko.
Mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 26 Februari 2025
yamelenga kujadili namna ya kutafuta amani katika mgogoro unaoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.