Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Kwagilwa: Serikali yahakikisha uchumi wa buluu unaleta manufaa kwa taifa

Aug, 20 2026

Serikali imesema inaendelea kuweka mkazo katika usimamizi na uendelezaji wa Sekta ya Uchumi wa Buluu ili iwe endelevu na yenye kuleta manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria cha kuwasilisha Mkakati wa utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu (2024-2034) kilichofanyika Dodoma Agosti 20, 2026.

Mhe. Kwagilwa alisema kuwa pamoja na hatua hiyo, Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imejipanga kuimarisha shughuli za uchumi wa buluu ikiendelea kuandaa Mpango wa Matumizi ya maeneo ya Maji ‘Marine Spatial Plan‘ (MSP).

Alisema Mpango huo utasaidia kubainisha maeneo ya kimkakati yatayochagiza katika shughuli zinazohusiana na sekta hiyo kwa kutekeleza Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu (2024) na Mkakati wake wa utekelezaji (2024 - 2034)

Aidha, Naibu Waziri Kwagilwa aliiarifu Kamati hiyo kuwa Tanzania inaendelea na maandalizi ya Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP12) utakaofanyika kuanzia Oktoba 06 hadi 09, 2026 jijini Dar es Salaam ambao pamoja na wadau mbalimbali pia utawahusisha Wabunge.

Akiongoza kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro pamoja na mambo mbalimbali alisisitiza Serikali iwajengee wananchi uelewa kuhusu masuala ya uchumi.

Alisema ni muhimu wananchi wajengewe uelewa ili watambue fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta hiyo kwani wengi wao wanadhani uchumi wa buluu unapatikana kupitia bahari pekee wakati wakati yapo maeneo mengine yakiwemo nishati, usafirishaji, utalii, madini, mazingira na viwanda.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Naibu Makatibu Wakuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Latifa Mohammed Khamis (Muungano), Dkt. Maduhu Kazi (Mazingira) pamoja na watendaji kutoka Ofisi hiyo.

Habari

Settings