Katibu Mkuu Maganga afungua kikao cha maandalizi ya COP28

Oct, 26 2023

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga amesema Serikali ya Tanzania imejipanga vyema katika Sera za utunzaji wa Mazingira kuendana na mabadiliko ya tabianchi katika maeneo nyeti ya Kilimo na Uchumi wa Buluu.

Amesema hayo wakati akifungua Kikao cha Kitaifa cha Wadau wa Maandilizi ya Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) utakaofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu kuanzia Novemba 30 hadi Decemba 12, 2023.

Bi. Maganga amesema kuwa amesema Serikali imeandaa Sera kuhusu masuala ambayo nchi inachangia katika kupunguza uzalishaji wa gesi joto hivyo COP28 itakuwa ni fursa kwa Tanzania kuieleza dunia mchango huo wa nchi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dkt. Omar Dadi Shajak amesema madhumuni ya kikao hicho ni kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa COP28 huku masuala ya Uchumi wa Buluu yatakuwa ni ajenda muhimu.

Nae, Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Paul Deogratius ametaja dhamira kuu ya wajumbe hao kukutana jijini Arusha ni kujadili kwa pamoja yaliyojiri kwenye COP27 iliyofanyika nchini Misri mwaka 2022 mafanikio, changamoto na mwelekeo kuelekea COP28.

Settings