Katibu Mkuu Luhemeja, Wajumbe Japan wafanya mazungumzo

Jun, 26 2025

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa ameambatana na ujumbe wa Wataalam wa Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Tanzania, amefanya mkutano wa uwili na ujumbe wa Serikali ya Japan, ambapo wamezungumzia namna bora ya kuimarisha ushirikiano kati ya Japani na Tanzania hususani katika biashara ya kaboni.

Mazungumzo hayo yalijikita katika ubainishaji wa utelekezaji wa makubaliano kuhusu biashara ya kaboni kati ya nchi hizo mbili.

Itakumbukwa kwamba mwezi Mei 2025 Tokyo, Japan, Serikali ya Japani na Tanzania zilisaini mkataba wa makubaliano ya kushirikiana katika utekelezaji wa miradi ya biashara ya kaboni.

Katika mkutano huo wa Uwili Ujumbe wa Serikali ya Japani uliwakilishwa Bw.Mitsuru Yamashiro kutoka Wizara ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi ya Japan, Bi. Mihoko Kawamura na Bw. Kentaro Takahashi kutoka Wakala wa Taasisi ya Biashara ya Kaboni Japan.

Aidha, katika mazungumzo hayo Serikali ya Tanzania na Japan zilikubaliana kuanza mara moja utekelezaji wa makubaliano hayo kwa kuunda Kamati zinazohitajika, kubainisha miradi ya kipaumbele katika utekelezaji kusaidia kujenga uwezo wa Watumishi na Miundombinu hitajika ya Kituo cha Taifa cha Biashara ya Kaboni (NCMC) pamoja na kuandaa na kuendesha mafunzo wa watalaam wa Tanzania kuhusu biashara.

Katika mkutano huo Mhandisi Luhemeja ameambatana na mkurugenzi wa Mazingira ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Kemilembe Mutasa, Wakurugenzi Wasaidizi wa Mazingira pamoja na Mwanasheria.

Settings