Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Dkt. Muyungi: Tutashirikiana na wadau kutekeleza Dira 2050

Feb, 23 2026

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi amekutana na kufanya mazungumzo na wataalamu kutoka Kampuni ya Vitol (World Largest EnergyTrader) na Vivo Energy.

Kikao hicho kimefanyika Februari 23, 2026 katika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.

Wataalamu wamemtembelea Katibu Mkuu kwa lengo la kupata mwongozo kuhusu biashara ya kaboni na kuchochea juhudi za erikali katika matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Akizungumza na wataalamu hao, Dkt. Muyungi ameishukuru kampuni hiyo kwa kutambua nafasi ya Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais katika usimamizi wa masuala ya uhifadhi wa mazingira hususani fursa zilizopo katika biashara ya kaboni.

Amesema Ofisi ya Makamu wa Rais ipo tayari kushirikiana na wadau mbalimbali katika eneo hilo muhimu linalotekeleza mchango wa Dira 2050.

Habari

Settings