Dkt. Kijaji: Tanzania kuandaa Mkakati wa Muda Mrefu wa Kaboni

Sep, 12 2024

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema Tanzania iko katika hatua za awali za kuandaa Mkakati wa Muda Mrefu wa Kaboni.

Amesema hayo wakati alipokutana na mabalozi wanaoziwakilisha nchi nne nchini ofisini kwake jijini Dar es Salaam kwa nyakati tofauti leo Septemba 12, 2024.

Akizungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Yasuhi Misawa, Mhe. Dkt. Kijaji amesema kuwa Serikali ina nia ya dhati katika kuelekea kwenye uchumi wa chini wa kaboni na kukuza mbinu za maendeleo endelevu.

Ameiomba Japan kushirikiana na Tanzania katika sema kuwa na kwa sasa iko katika utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Kupika Safi 2024-20234 ambao gharama yake ni takriban Dola za Kimarekani bilioni 1.8 (shilingi za trilioni 4.6).

Pia, ameiomba Serikali ya nchi hiyo kuimarisha uwezo wa Kituo cha Kitaifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) na kuongeza uwezo wa kiufundi kwa ajili ya kufanya Tathmini ya Athari za Mabadiliko ya Tabianchi.

Akizungumza na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud Al Shidhani, Waziri Mhe. Dkt. Kijaji amesema Tanzania imechukua hatua zote kuhakikisha inakabiliana na athari za kimazingira.

Settings