Wasifu

Mhe.Khamis Hamza Khamis
Mhe. Khamis Hamza Khamis
Naibu Waziri (Muungano na Mazingira)

Mhe. Khamis Hamza Khamis amehitimu Shahada ya Kwanza ya Sheria na Sharia kutoka Chuo Kikuu cha Zanzibar, Stashahada ya Elimu kutoka Chuo cha Ualimu cha Nkrumah.

Ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Mwenyekiti wa Rasilimali Watu wa Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji na Zimamoto.

Pia, Mhe.Khamis alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Naibu Mwenyekiti wa Bunge. Rasilimali Watu Pamoja kwa Polisi, Magereza, Uhamiaji na Zimamoto na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani.

Mhe. Khamis Hamza Khamis ni mbunge wa Tanzania kuanzia mwaka 2020 hadi sasa akiwakilisha Jimbo la Uzini. Aliteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kuanzia 2022 hadi sasa, pia aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuanzia mwaka 2020 hadi 2022.

Settings