Wasifu
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango
Makamu wa Rais, 2021 - 2025
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango alizaliwa tarehe 14 Julai 1957. Ni Mchumi na mwanasiasa kutoka Tanzania ambaye aliwahi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 2021 hadi 2025.
Aliapishwa tarehe 31 Machi 2021 kushika wadhifa huo baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na kabla ya hapo, aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



