Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Taasisi za elimu zaunga mkono matumizi ya nishati safi

Sep, 21 2026

Taasisi za elimu zimeendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa hivyo kupunguza vitendo vya ukataji wa miti.

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi katika Shule ya awali na Msingi ya Kingereza Hosiana iliyopo Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

Akizungumza wakati wa mahafali ya darasa la saba 2026 Dkt. Muyungi alipongeza uongozi wa shule hiyo kwa kubuni mradi wa nishati safi ya kupikia ambao unasaidia kuendeleza kampeni ya utunzaji wa mazingira.

Alisema aina ya teknolojia inayotumika katika mapishi ni mfano wa kuigwa kwani immeokoa miti 1,800 kwa mwaka kwa mujibu wa taarifa ya shule hivyo itachangia kutimizi azma ya Serikali ya kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishatin safi nifipakpo mwaka 2034.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Bw. Isaya Tendega alisema kuwa Serikali ya mkoa huo wa itaendelea kushirikiana na shule hiyo katika kukuza maendeleo ya sekta ya elimu.

Nae Mkurugenzi wa shule hiyo ya Hosiana, Shadrack Ntimba alisema kuwa mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari ambao umezinduliwa na Dkt. Muyungi umegharimu zaidi ya shilingi bilioni moja.

Itakumbukwa kuwa Serikali ilitangaza kusitisha matumizi ya kuni na mkaa kwa taasisi zote za umma na binafsi Tanzania Bara zinazoandaa chakula na kulisha watu zaidi ya 100 kwa siku kusitisha matumizi ya kuni na mkaa kuanzia Januari 31, 2024.

Hatua hiyo inasaidia kuokoa mazingira kwakuwa inapunguza vitendo vya ukataji wa miti kwa ajili ya nishati hiyo chafu sanjari na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Habari

Settings