Makamu wa Rais ashiriki Mkutano AU-EU Summit

Nov, 24 2025

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameshiriki katika ufunguzi wa Mkutano wa 7 wa Viongozi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya (AU-EU Summit), unaofanyika Jijini Luanda nchini Angola.

Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo unaadhimisha miaka 25 ya ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika.

Mkutano huo unafanyika chini ya kauli mbiu isemayo “Kukuza amani na ushirikiano kupitia Ustawi wa Kimataifa wenye Tija” (promoting peace and prosperity through effective Multilateralism)

Katika Mkutano huo, Makamu wa Rais ameambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Kazi, Uchumi na Uwekezaji Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Sharif Sharif, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt. Ngwaru Maghembe, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Afrika Mhe. Balozi Innocent Shiyo, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Umoja wa Ulaya Mhe. Balozi Jestas Nyamanga, pamoja na wataalamu mbalimbali.

Settings