Habari
Dkt. Muyungi: Serikali kuendelea kutafuta fedha za kukabili mabadiliko ya tabianchi
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi amesema ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, Serikali itaendelea kutafuta fedha kutoka Mifuko ya Mazingira na mikataba mbalimbali kimataifa.
Akizungumza wakati akifungua Mkutano na Taasisi Wakala wa Mfuko wa Dunia wa Hifadhi ya Mazingira (GEF) jijini Dodoma leo Januari 30, 2026, Dkt. Muyungi amesema mabadiliko ya tabianchi yanahitaji rasilimali fedha, utalaamu na ushirikishwaji wa wadau maendeleo duniani.
Amesema kuwa pamoja na hatua mbalimbali za nchi katika kukabiliana na changamoto hiyo, elimu ya kutekeleza miradi mi muhimu kama nchi hivyo Ofisi ya Makamu wa Rais imeendelea kuwajengea uwezo wataalamu watakaosaidia katika kufuatilia upatikanaji wa fedha hizo.
Dkt. Muyungi alisema kuwa kuna kazi ya kuhakikisha upatikanaji wa fedha hizo unakuwa wa haraka bila kusuasua ili kuhakikisha zinatumika vyema kwa ajili ya utekeelzaji wa miradi ya ya mazingira ili ilete manufaa kwa wananchi.
“Mara nyingi tunapohitaji fedha zinachelewa kupatikana na hivyo kuchukua muda mrefu kwenda kwa wananchi, sisi kama Ofisi ya Makamu wa Rais tunao wajibu wa kuhakikisha tunaisaidia nchi kuhakikisha miradi inatekelezwa,” alisema.
Aidha, Dkt. Muyungi alisema kuwa Serikali ya Tanzania inatambua mchango mkubwa wa GEF katika ajenda ya maendeleo ya taifa, hususan katika kuendeleza uhifadhi wa mazingira, ulinzi na ustahimilivu wa tabianchi, hivyo
Aliongeza kuwa Ushirikiano wet umewezesha nchi kupata maendeleo makubwa katika kushughulikia changamoto kuu za mazingira, zikiwemo uharibifu wa ardhi, upotevu wa viumbe hai, athari za mabadiliko ya hali ya hewa, viumbe ngeni vamizi, uchafuzi wa mazingira, na uharibifu wa mifumo ikolojia ya majini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Bi. Farhat Mbarouk aliishukuru Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusema Zanzibar inafaidika na miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa GEF.
Alisema kuwa kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) umeleta matunda katika Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Mkoa wa Kaskazini kwani umewawezesha wananchi kujipatia kipato kutokana na shughuli za utunzaji wa mazingira.
Awali akitoa neno la utangulizi, Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Thomas Chali alisema lengo la mkutano huo ni kupokea taarifa za Taasisi wakala kuhusu miradi inayotekeelzwa.
Alisema kupitia mkutano wadau hao watabadilishana uzoefu wa namna ya usimamizi unavyotekelezwa hasa ukzingati wakati huu ambapo maandalizi yanafanyika kuhusu awamu ya tisa ya utekelezaji wa miradi.



