Waziri Zungu aahidi wananchi Serikali kujenga dampo la kisasa Dar

Jan, 30 2020

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu amesema Serikali inatarajia kujenga dampo la kisasa katika Mkoa wa Dar es Salaam ili liweze kuhimili taka zote zinazozalishwa mkoani humo.

Zungu amesema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kawe Mhe. Halima Mdee aliyeuliza kuwa Serikali ina mkakati gani wa kujenga madampo mengine katika wilaya zote za mkoa huo kwani hivi sasa kuna dampo moja la Pugu Kinyamwezi.

Alibainisha kuwa kiasi cha sh. bilioni 75 zimetolewa na wafadhili kwa ajili ya kazi hiyo ambayo itakwenda sambamba na ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami katika eneo la dampo ili kurahisha usafirishaji wa taka ambapo Halmashauri ya Jiji hilo imetenga fedha. “Kasi ya taka zinazozalishwa Dar es Salaam ni kubwa na jiji linakua kwa asilimia kubwa sana na kwa miaka miwili ijayo kasi ya population itafika milioni 8 hadi 9 na dampo ni moja na juzi mimi nimetembelea, dampo hali ya dampo ni mbaya lazima tukiri ni mbaya miundombinu ni mbaya hatua zimeshachukuliwa,” alisema Zungu.

Settings