Waziri Jafo atoa maelekezo kwa wataalamu kunusuru wananchi wa Pangani

Jan, 16 2022

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo amefanya ziara katika Wilaya ya Pangani mkoani Tanga leo Januari 16, 2022 changamoto ya kuliwa kwa ukuta unaotenganisha maji ya Mto Pangani na eneo la Bweni wilayani Pangani mkoani Tanga.

Akiwa katiia ziara hiyo Dkt. Jafo ametoa maelekezo kwa kwa afisa mazingira wa wilaya na mkoa kwa kushirikiana na wataalamu wa ujenzi kufanya tathmini ya namna gani ya nini kifanyike ili Serikali iweze kutafuta fedha kuwanusuru na changamoto hiyo inayotishia kulimeza eneo hilo.

“Hili jambo nimelichukua na niwaahidi nitaenda kulifanyia kazi na natoa mwezi mmoja kwa afisa mazingira kwa mkoa na wilaya pamoja na mainjini muende mkafanye tathmini ni kiasi gani cha fedha kitahitajika ili kuparekebisha mahali hapa,” alisema.

Aidha, Waziri Jafo alisema kuwa eneo hilo lina changamoto kubwa kiasi cha kuweza kuhatarisha maisha ya wananchi na hata pengine kutishia kukatisha mawasiliano ya barabara wakati wa kipindi cha bamvua.

Alipongeza na kushuruku taasisi wilayani humo kwa kushirikiana na Serikali kupanda mikoko kando ya Mto Pangani kiasi cha takriban 24,000 zaidi ya lengo la 21,000 walilojiwekea.

Waziri huyo alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi waitunze mikoko hiyo ili iweze kuwa na manufaa hususan katika kusaidia jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wake Afisa Mazingira wa Wilaya ya Pangani, Bw. Daudi Mlahagwa akiwasilisha taarifa ya mazingira alisema wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto ya vyanzo vya maji.

Alibainisha kuwa miongoni mwa changamoto hizo ni kukauka kwa baadhi ya vyanzo hivyo, wafugaji kuingiza mifugo katika vyanzo na hivyo kuviharibu, visima vifupi kukauka kutoka na joto kali na chumvi kuingia katika visima na kusababisha kutokufa kwa matumizi ya binadamu.

Settings