Wawekezaji viwanda watakiwa kuzingatia hifadhi ya mazingira

Apr, 06 2024

Wawekezaji wa viwanda na miradi mbalimbaliza ya maendeleo wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuhakikisha wanazingatia utunzaji na ulindaji wa mazingira katika eneo linalowazunguka.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Bw. Raymond Mangwala amesema hayo wakati wa ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Aprili 5,2024 katika wilaya hiyo.

Bw. Mangwala alitolea mfano Mradi wa Tofali za Mwamba (Rock Block) uliopo Horiri ambao baada ya kukamilika kwa mradi huo wawekezaji wataweka bwawa la kufugia Samaki pamoja na mradi wa maji kwa ajili ya jamii inayozunguka eneo hilo.

“Tayari tumeshawaelekeza wawekezaji wa mradi huu katika utunzaji wa mazingira na hapa watageuza eneo hili na kuwa bwawa la Samaki na kitakuwa chanzo cha maji.

“Tumeshakaa nao na kuliona hilo kuhakikisha mazingira yanabaki kuwa salama muda wote,” amema Bw. Mangwala.

Kwa upande wake, Meneja wa Mradi huo, Bw. Fabian Oisso amesema wataendelea kufuatilia ushauri wa wataalamu kila wakati ili kuhakikisha wanatunza mazingira.

Mradi huo umekuwa ukizalisha tofali za miamba baada ya kuchongwa kwa mawe yanayochimba katika eneo hilo.

Settings