Waitara awataka wafanyabiashara wa vyuma chakavu kutojihusisha uhujumu wa miundombinu

Dec, 22 2020

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Mwita Waitara amewataka wafanyabiashara wa chuma chakavu kuwa waaminifu na kuepuka kujihusisha kuhujumu miundombinu.

Waitara ametoa kauli hiyo leo Desemba 22, 2020 alipofanya kikao na wafanyabiashara hao jijini Mwanza ambapo alionya pamoja na Serikali kuitambua biashara hiyo lakini wapo baadhi ya watu wanaharibu miundombinu na kuwauzia kama chuma chakavu kinyume cha sheria.

Aliwataka wafanyabiashara hao kufanya kazi na Serikali katika kuwafichua wanaoharibu miundombinu kisha kuwauzia kama vyuma chakavu kwani kitendo hicho ni sawa na uhujumu uchumi na wanachafua jina lenu.

“Ukifanya kazi kwa mujibu wa sheria hautagombana na mtu yeyote wa Serikali, umepewa kibali cha kununua chuma chakavu kiwe chakavu kweli na anayekuuzia lazima umfahamu ili tukifuatilia tusikupe mzigo huo na mjua kabisa hili ni jambo baya na kuna wenzenu walikamatwa na wapo katika hatua za kuwajibishwa,” alionya.

Aidha, Naibu waziri aliongeza ipo haja ya kumshauri Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais ambaye ndiye mwenye dhamana ya vibali tupitie upya vibali hivyo na ikibainika wafutiwe akisema kuwa ni kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Awali akitembelea kiwanda cha kurejeleza chupa za plastiki cha Falcon jijini Mwanza alipongeza jitihada za mwekezaji huyo kwa kusaidia kusafisha mazingira kwa kukusanya chupa hizo.

“Naomba niwapongeze sana kwani tutakumbuka tarehe moja Juni wakati tulipopiga marufuku mifuko ya plastiki mzigo wa tani takriban nane ulisalimishwa.

“Mnasaidia sana kusafisha mazingira na mnatoa ajira maana yake wananchi wakikusanya chupoa hizi wanapata chochote ni ajira hii na nimefurishwa sana mnazalisha product zingine naona benchi haoa meza badala ya kukata miti na kuharibu mazingira,” alisema.

Settings