Serikali: Utatuzi wa changamoto za Muungano ni wa mafanikio

Nov, 03 2023

Serikali imesema inaangalia uwezekano wa kufanya vikao vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kuwa vya kisheria.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati akijibu maswali bungeni jijini Dodoma leo Novemba 3, 2023.

Amesema kuwa changamoto zote za Muungano zimekuwa zikitatuliwa na kupatiwa ufumbuzi kwa njia ya majadiliano na maridhiano, utaratibu ambaoi umekuwa wa mafanikio makubwa.

Mhe. Khamis amesema kuwa katika utatuzi wa changamoto hizo umeandaliwa utaratibu wa vikao vya Kamati ya Pamoja ya SJMT na SMZ wa kushughulikia masuala ya Muungano wa Aprili 2019.

Akiendelea kujibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mwera Mhe. Zahor Mohammed Haji, Naibu Waziri Khamis amesema kuwa utaratibu wa vikao hivi umetumika kwa mafanikio makubwa na kuhakikisha changamoto nyingi zinatatuliwa.

Settings