Dkt. Mkama afungua warsha kwa maafisa wa Serikali Tunduma

Jan, 13 2023

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dkt.Switbert Mkama,leo amefungua Warsha ya mafunzo kwa Maafisa wa Serikali waliopo Katika mpaka wa Tunduma.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Bi.Catherine Bamwezaki,amesema kuwa

Warsha hii inalenga katika kujenga uwezo kuhusu udhibiti wa uingizaji nchini wa kemikali zinazomong'onyoa tabaka la Ozoni.

Wahudhuriaji wa Warsha hii ni wadau mbalimbalj kutoka Ofisi ya Rais, Wizara ya Mifugo, Uvuvi,Afya,kilimo,Mamlaka ya Mapato Tanzania,Uhamiahi, Jeshi la polisi,TBS,Mamlaka ya Maabara ya MkemiaMkuu wa Serikali,Wakala wa Vipimo Tanzania, Wakala wa Meli,TMDA,Wakala wa Wanyama pori,Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania pamoja na Baraza la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira.

Akifungua kikao hichoNaibu Katibu Mkuu,ameeleza, kuwa Mafunzo haya ni Muhimu sana kwan mwanzoni mwa miaka ya 70 wanasayansi walivumbua kwamba baadhi ya kemikali zinazotengenezwa na binadamu hujipenyeza angani na kumong'onyoa Tabaka la hewa ya Ozoni.

Aidha uchunguzi wa angahewa tangu miaka hiyo umethibitisha kwamba Tabaka la Ozoni limekuwa likimong'onyoka kwa Kasi ya 5% kila muongo.

Matokeo ya kumong'onyoka kwa Tabaka la Ozoni ni kuruhusu mionzi zaidi ya urujuani kufikia uso wa dunia ambayo husababisha madhara mbalimbali kwa afya ya binadamu na Mazingira.

Madhara hayo ni kama vile magonjwa ya saratani ya ngozi,uharibifu wa macho unaosababisha upofu na athari kwa ukuaji wa mimea na viumbe hai wengine.

Akitaja Kemikali hizo Dkt.Mkama amesema " kemikali zinazoharibu Tabaka la Ozoni ni kemikali/ gesi zinazotumika Katika majokofu na viyoyozi mbalimbali,vifaa vya kuzimia moto,usafishaji chuma,utengenezaji magodoro,ufukizaji wa udongo Katikavitalu vya tumbaku na kilimo cha maua, hifadhi ya nafaka Katika maghala na kadhalika.

Kemikali hizi huingizwa nchini kupitia mipaka mbalimbali kwa ajili ya Matumizi tajwa hapo juu".

Hivyo,kutokana na Matumizi na madhara ya kemikali hizo Serikali inawataka wasimamizi wa sheria mipakani kuendelea na usimamizi na udhibiti wa Kemikali zinazodhibitiwa Kwa kuzingatia ukomo wa Matumizi wa kemikali hizo.

" Ni matumaini yangu kuwa,kupitia Warsha hii mtajengewa uelewa Mkubwa zaidi Katika masuala ya Tabaka la Ozoni na hatimae kuwa mabalozi wa kueneza elimu ya Ozoni kwa wengine Ili sote kwa pamoja tuongeze juhudi za kuhifadhi Tabaka la Ozoni, na hivyo kuokoa maisha ya dunia" ,Dkt Mkama .

Akishukuru kwa niaba ya wadau wengine.Kaimu meneja Msaidizi wa Forodha Songwe Bw. Joseph Maleko,amesema kuwa Mafunzo haya ni Muhimu sana kwani yanawajengea uelewa Kuhusu Kemikali hizo na hivyo kurahisisha utekelezaji na utendaji Kazi Katika udhibiti wa uingizaji wa Kemikali hizo nchini.

Warsha hii ya siku mbili inafanyika Tunduma Mkoani Songwe.

Settings