Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akisoma hotuba kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani leo Juni 5, 2020 jijini Dodoma yaliyoambatana na ufungaji na utoaji vyeti kwa wakaguzi wa mazingira kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa za Mkoa wa Dodoma. Kaulimbiu ya mwaka huu ni “Tutunze Mazingira: Tukabiliane na Mabadiliko ya Tabianchi”.