WAKAGUZI WA BIO-TEKNOLOJI YA KISASA WAPEWA MAFUNZO

Katika jitihada za kuendelea kukuza uelewa wa wadau na jamii nzima kuhusu matumizi salama ya teknolojia ya uhandisi jeni /bio-teknolijia ya kisasa, Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Shirika la NEPAD chini ya Umoja wa Afrika hii leo wamefanya mafunzo kwa wataalamu kutoka  Wizara na Taasisi za Serikali kuhusu Usimamizi wa Matumizi Salama ya Teknolojia ya kisasa katika ngazi ya Utafiti (Management on Confined Field Trial for GM Crops)

Mafunzo hayo ya siku mbili yanafanyika jijini Dodoma na yamefunguliwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine, na kufuatiwa na mafunzo kwa vitendo katika kituo cha Utafiti wa Kilimo Makutopora, Dodoma