Viongozi wa watakiwa kuunga mkono Uchumi wa Viwanda

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. SamiaSuluhu Hassan amewataka viongozi wa Dini nchini kuunga mkono azma ya Serikali ya kujenga uchumi wa viwanda.

MakamuwaRais ameyasema hayo wakati wa Ibada ya Kuzindua Dayosisi ya Magharibi Kati na kumuweka Wakfu na Kumuingiza kazini Askofu Mteule Mchungaji Dkt. Isaac Kissiri Laiser na kuingizwa kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Newton John Maganga katika Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri Tabora.

Makamu wa Rais amesema hivi karibuni Serikali imepitisha mabadiliko na mpango mpya wa uwekezaji Tanzania.

Makamu wa Rais amesema kuwa kudumisha Amani nausalamanijukumu la wote“ Endeleeni kuhubiri Amani na kwa upande wa Serikalini wahakikishie Watanzania Wote kwamba Amani na Usalamani kipaumbele chetu hatutavumilia kumstahimilia mtu yeyote yule ambaye ana lengo la kuharibu Amani ya Tanzania hatutamvumilia tutamshughulikiai pasavyo”

Makamu wa Rais amesema“Tukosoeni pale tunapokosea nasi tunawaahidi tutarekebisha na twende mbele kwani Mwalimu Nyerere alituambia kuongoza nikuonyesha njia na katika kuonyesha njia lazima ukubali kukosolewa na si tunakubali kukosolewa hilo nalo ni jukumu la utumishi wa kiroho kwa hiyo endeleeni kutukosoa kwa ile lugha ambayo tutafahamiana”

Makamu wa Rais amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Taasisi za dini katika masuala ya maendeleo na kuboresha huduma za kijamii.

Makamu wa Rais amelishukuru na kulipongeza Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kwa mchango wake mkubwa unatoa katika nchi yetu hususani katika Nyanja za Elimu, Huduma za Afya na Maji.

Nae AskofuMkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Baba Askofu Fredrick Shoo amesema kuwa wanaona jitihada za Mheshimiwa  Rais na wataendelea kumuunga mkono na wapo pamoja kushirikiana na Serikali kwania njema kabisa.