TAARIFA KWA UMMA: KIKAO CHA WADAU WA MIFUKO MBADALA YA PLASTIKI

TAARIFA KWA UMMA

Matumizi ya mifuko ya plastiki yana athari katika mazingira kwa kuwa haiozi. Katika utekelezaji wa agizo la  Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa la kupiga marufuku mifuko ya plastiki, Ofisi ya Makamu wa Rais inapenda kuwaalika Wadau wote wanaojihusisha na uzalishaji, uuzaji na usambazaji wa  mifuko mbadala wa plastiki (mifuko rafiki wa mazingira) kushiriki katika kikao kitakachofanyika jijini Dar Es salaam katika Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC).

Siku: Jumatatu

Tarehe: 15/04/2019.

Muda: Saa 2:00 (mbili kamili) asubuhi

Mgeni Rasmi: Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba.

Kwa maelezo zaidi piga simu  kwa:

Bi. Geneva Orengeile 0759 020727

Bi. Suzan Chala          0652 134313

 

WOTE MNAKARIBISHWA