TAARIFA KWA UMMA

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA MAKAMU WA RAIS

 

 

 

TAARIFA KWA UMMA

Ofisi ya Makamu wa Rais inapenda kuwataarifu wananchi kuwa taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii inayosema: “MIFUKO YA PLASTIKI KUENDELEA KUTUMIKA KWA SASA” si sahihi. Katazo la Matumizi ya mifuko ya plastiki linabaki kuwa tarehe 01 Juni 2019 kama ilivyotangazwa na Serikali hapo awali. Ikumbukwe kuwa adhabu kwa wazalishaji, wauzaji na watumiaji wa mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku kutumika kwa wote watakaokaidi.

Ofisi ya Makamu wa Rais inawaasa watanzania kuchukua tahadhari ya matangazo ya aina hiyo na inapotokea wasiliana nasi kwa namba ya simu ifuatayo: 0685 333 444

 

 

Lulu Mussa

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Ofisi ya Makamu wa Rais

10/05/2019