TAARIFA KWA UMMA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA MAKAMU WA RAIS

TAARIFA KWA UMMA

UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA BARAZA LA TAIFA LA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA – NEMC

Kufuatia uteuzi uliofanywa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wa kumteua Prof. Eng. Esnati Osinde Chaggu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira – NEMC na kumteua Dkt. Samwel Gwamaka kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira – NEMC, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mheshimiwa January Y. Makamba (Mb.) amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira – NEMC kwa kipindi cha miaka mitatu (3).

  • Flora Ismail Tibazarwa
  • Hussein Sosovele
  • Catherine Aloyce Masao
  • Ndugu Damas Augustine Masologo
  • Neduvoto P. Mollel
  • Dos Santos Aristaricky Silayo
  • Mwakalukwa Ezekiel Edward
  • William Mwegoha

Vilevile, Mheshimiwa Waziri January Y. Makamba (Mb.) amemteua Prof. William Mwegoha kuwa Mkurugenzi wa Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais.

 

Mhandisi Joseph K. Malongo

KATIBU MKUU

17 Desemba, 2018