Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea vituo vya kufua umeme kwa maji ya mabwawa ya Mtera na Kidatu kukagua hali ya maji na athari za mazingira zinazotokana na mvua zinazoedelea kunyesha nchini. Kushoto ni Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare