Miradi na programu za maendeleo zinazotekelezwa pande mbili za Muungano zanufaisha wengi

Idara ya Muungano chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais hivi karibuni imewakutanisha Waratibu wa miradi na programu za maendeleo zinazofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mgeni rasmi katika kikao kazi hicho Mhasibu Mkuu Bw. Paschal Karomba alisema kikao hicho kilijikita katika mambo makuu mawili, kupata taarifa ya utekelezaji wa miradi na programu za maendeleo na  kukubaliana namna bora ya upatikanaji wa taarifa za utekelezaji.

Miradi na programu zinazoendelea kutekelezwa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar  ni pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tanzania Social Action Fund – TASAF III ); Mradi wa Kuongeza Tija na Uzalishaji wa Zao la Mpunga (Expanded Rice Production Project – ERPP); Mradi wa Kujenga Uwezo wa Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi katika Maeneo ya Pwani- LDCF; Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania   (MKURABITA).

Aidha, Programu nyingine ni Programu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Fedha Vijijini  (Market Infrastracture, Value Addition and Rural Finance – MIVARF); Mradi wa Udhibiti wa Uvuvi na Maendeleo Shirikishi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi – SWIOFISH.

Pia Mradi wa Upanuzi wa Usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania na Mradi wa Uboreshaji wa Elimu kupitia Global Partnership for Education, pamoja na Tanzania Initiatives for Preventing Aflatoxin Contamination – TANIPAC na Public Financial Management Reform Programe – PFMRP.