Sekretarieti ya SMT na SMZ yakutana Dodoma

?Sekretarieti ya Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ((SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ya kushughulikia masuala ya Muungano imekutana leo Julai 6, 2020 jijini Dodoma.

Kikao hicho kimeongozwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Joseph Sokoine na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hassan Abdallah Mitawi.

Pamoja na mambo mbalimbali lengo la kikao hicho lilikuwa ni kufanya maandalizi ya Kikao kijacho cha kitakachohusisha Kamati ya Pamoja ya Serikali hizo mbili.

Aidha, Sekretarieti hiyo inaundwa na wajumbe wanane kutoka Tanzania Bara na wanne kutoka Zanzibar ambapo viongozi hao wamewawakilisha Katibu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Joseph Malongo na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Seif Shaaban Mohamed.

 

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo (katikati) na Naibu Katibu Mkuu wake Balozi Joseph Sokoine wakibadilishana mawazo na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano) Dkt. Zainab Chaula nje jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma mara baada ya kumaliza Kikao cha pamoja cha