Sekretarieti ya SMT na SMZ yakutana Dodoma kujadili Muungano

Sekretarieti ya Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ((SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ya kushughulikia masuala ya Muungano imekutana leo Julai 6, 2020 jijini Dodoma.

Kikao hicho kimeongozwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Joseph Sokoine na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hassan Abdallah Mitawi kwa niaba ya Katibu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Joseph Malongo na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Seif Shaaban Mohamed.

Pamoja na mambo mbalimbali lengo la kikao hicho lilikuwa ni kufanya maandalizi ya Kikao kijacho cha g ya Pamoja ya Serikali hizo mbili ambacho hutanguliwa na vikao vya Makatibu Wakuu wa SMT na SMZ na kikao cha Mawaziri wa SMT na SMZ.

Aidha, Sekretarieti hiyo inaundwa na wajumbe wanane ambapo wannne ni kutoka Tanzania Bara na wanne kutoka Zanzibar.