MAKAMU WA RAIS AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI SONGWE NA KUINGIA MKOANI MBEYA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan awewataka Viongozi wa mkoa wa Songwe kuwa na ushirikiano baina ya Uongozi.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo kwa siku 5 mkoani Songwe.

Makamu wa Rais amesema kuwa kuna changamoto ya Utawala bora ndani ya Halmashauri hivyo kuutaka uongozi wa mkoa kutoa mafunzo ya utawala bora katika ngazi ya Halmashauri.

Makamu wa Rais amevutiwa sana na shughuliza ujasiriamali na kuutaka Uongozi wa mkoa huo kuwasaidia Wajasiriamali hao.

Makamu wa Rais ameuagizaUongozi wa mkoa kuanzisha program maalum ya kupima afya wakazi wa mkoa huo huku akiweka msisitizo juu ya elimu ya afya na uzazi wa mpango.

Makamu wa Rais amehimiza sana kutunza mazingira na kupanda miti kwa wingi.

Mara baada ya kikao hicho Makamu wa Rais alielekea mkoani Mbeya ambapo alipokelewa na mamia ya watu katika eneo la Mbalizi.

Makamu wa Rais aliwasalimu wakazi wa Mbalizi na kuwapa pole kwa ajali zinazotokea mara kwa mara kwenye eneo la mteremko Mbalizi.

Makamu wa Rais aliwaambia wananchi hao kuwa tayari serikali imeanza kushughulikia changamoto za miundombinu za barabara ambapo bara bara ya mchepuko inajengwa ili kupunguza ajali katika mteremko huo korofi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka wananchi kuendelea kutunza Amani na Utulivu na kuahidi kutekelezwa kwa ahadi zote zilizotolewa.