Mafunzo ya Msasa ya wawezeshaji shamba darasa mradi wa LDSF yaingia siku ya pili Morogoro

 

Mafunzo ya Msasa ya Uwezeshaji kuhusu Mashamba darasa kwa Maafisa Viungo wa Mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame nchini (LDSF) yameendelea leo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo mkoani Morogoro ikiwa ni siku ya pili. Pichani washiriki wa mafunzo hayo wakijadili masuala ya mabadiliko ya tabia nchi katika makundi.
Mafunzo hayo yalifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine.