KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS AONGOZA OPARESHENI YA UKAGUZI WA MIFUKO YA PLASTIKI JIJINI DODOMA

 

Wito umetolewa kwa Wakazi wa Dodoma na Wilaya zake  kuacha kabisa kautumia mifuko ya plastiki na kuanza mara moja matumizi ya mifuko mbadala ikiwa ni kutii agizo la Serikali la kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Injinia Joseph Malongo wakati wa uzinduzi wa operesheni ya kukagua mifuko ya plastiki katika jiji la Dodoma ambapo ni kutii agizo la Serikali la ukomo wa matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia juni 1.

Akiongea katika oparesheni hiyo amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais ndiyo Wasimamizi wakubwa wa mazingira Nchini, hivyo amefurahi kuona elimu juu ya katazo la mifuko ya plastiki kwa jiji la Dodoma imefika kwa Wananchi kwa sababu ambao wamekutwa na mifuko ya plastiki ni wachache sana kulinganisha na Wananchi wanaotumia mifuko mbadala kwa siku ya leo. ‘Elimu imefika kwani kila Mwananchi namuona kabeba mfuko mbadala, vikapu n.k” alisema Injinia Malongo

Naye Mkuu wa Wilaya wa jiji la Dodoma Mh. Protabas Katambi amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu na anawaagiza Wananchi na Wafanyabiashra wa jiji laDodoma  kutii agizo la Serikali na kuachana kabisaa na matumizi ya mifuko ya plastiki. ‘Mwananchi atakayekutwa na mfuko wa plastiki hatua kali za kisheria zitachukuliwa juu yake, hili suala syo mchezo mchezo nia agizo la Serikali” alisema Katambi

Operesheni hiyo ya kukagua mifuko ya plastiki imekuja baada ya Waziri Mkuu wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa kutoa agizo bungeni kuwa ifikapo juni 1 hakuna Mwananachi atakayeruhusiwa kutumia mifuko ya plastiki Nchini Tanzania.