FURSA ZA KUNUFAIKA NA MFUKO WA MAZINGIRA WA DUNIA- GEF

FURSA ZA KUNUFAIKA NA MFUKO WA MAZIGIRA WA DUNIA- GEF

1.    UTANGULIZI

Mfuko wa Mazingira Duniani (Global Environment Facility –GEF) ulianzishwa mwaka 1991. Lengo la Mfuko huu ni kutoa fedha kwa nchi zinazoendelea na zinazoinukia kiuchumi, ambazo ni wanachama wa mikataba mabalimbali ya kimataifa ya mazingira kwa ajili ya kugharamia shughuli/miradi mbalimbali ya kukabiliana na changamoto sita za mazingira  ambazo zimeonekana kuwa ni tishio kwa Dunia. Changamoto hizo ni (1) Kupotea kwa Bioanuai Duniani (Loss of Biodiversity); (2) Mabadiliko ya Tabianchi (Climate Change); (3) Uharibifu wa Ardhi (Land degradation); (4) Uchafuzi wa Maji ya Kimataifa (International Waters’ Pollution); (5) Kumong’onyoka kwa tabaka la Ozoni (Ozone Layer Depletion); na (6) Uharibifu unaotokana na kemikali zinazodumu kwa muda mrefu kwenye Mazingira (Persistent Organic Pollutants). Wachangiaji wakubwa wa mfuko huu ni nchi zilizoendelea ambazo kwa kiasi kikubwa maendeleo yake yamechangia katika uharibifu wa mazingira ambao ni mjadala mkubwa katika ulimwengu wa sasa.

2.    TANZANIA INAVYONUFAIKA NA MFUKO WA MAZIGIRA WA DUNIA

Fedha kutoka GEF hulenga kusaidia utekelezaji wa vipengele vya miradi au programu chini ya  mikataba hii ambavyo visingetekelezeka katika mipango ya kawaida ya maendeleo ya nchi husika (environmentadditional and incremental costs). Hizi ni  gharama ambazo zisingekuwepo bila uharibifu wa mazingira. Mfuko huu huwa unatoa fedha kwa nchi wanachama kwa awamu ambayo ni kila baada ya miaka minne kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya mazingira hapa nchini. Tangu GEF ianze mpaka sasa Tanzania tumenufaika kwa kutekeleza miradi mbalimbali inayofadhiliwa na GEF chini ya mikataba ya kimataifaya mazingira ambayoTanzania ni mwanachama.

3.    HATUA INAYOFUATA

Kwa kipindi cha miaka minne ijayo (2018-2022) GEF imeipatia Tanzania Jumla ya Dolaza Kimarekani milioni 24 kwaajili ya kutekelezamiradimbalimbali ya mazingira hapa nchini. Ofisi ya Makamu wa Rais nawataka Wizara kwa kushirikiana na Taasisi za serikali kuandaa maandiko ya miradi (concept note) mazingira yanayolenga maeneo yaliyotajwa hapo juu kwa ajili ya ufadhili wa Mfuko huu. Mwisho wa kuwasilisha maandiko hayo ni mwezi Desemba, 2018. Aidha, Ofisi ya Makamu wa Rais itawajulisha tarehe ya kuwa na kikao cha wadau kwa ajili ya kujadili maandiko hayo. Kwa tarifa zaidi tafadhali wasiliana na Bi. Fainahappy Kimambo kwa simu namba. 0754 868 305 au Bw. Thomas Chali kwa simu namba 0717 086 610.