ZIARA YA MAKAMU WA RAIS KAMPASI YA MLOGANZILA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema ufumbuzi umepatikana wa changamoto kubwa ya umeme inayoikabili hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila na kuahidi kusimamia utendaji ili umeme upatikane muda wote.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila.

Makamu wa Rais amesema kwa vifaa vya kisasa vya umeme vilivyopo hospitalini hapo havipaswi kupata umeme wa mashaka .

Makamu wa Rais amesema kuwa wananchi wengi hawajajua umuhimu wa kuwa na bima ya afya hivyo elimu zaidi itolewe ili wananchi wengi wachangie huduma ya afya kwa kupitia bima zao hii itawapunguzia gharama sana wakati wa matibabu.

Makamu wa Rais ameutaka uongozi wa Mloganzila kutangaza kwa wananchi huduma zinazopatikana hospitalini hapo ambapo wana vifaavya kisasa kabisa kwa ajili ya uchunguzi wa afya, Makamu wa Rais alisema huduma ya kupima saratani ya matiti katika hospitali ya Mloganzila ni shilingi elfu 30 tu.

Akiongea na Watumishi wa hospitali hiyo Makamu wa Rais amesema “Mnaofanya kazi sekta ya afya mnafanya kazi ya Uungu”

Makamu wa Rais  pia aliwasikiliza wananchi waliofika kupata huduma hospitalini hapo na kusema kuwa Serikali itajitahidi kushughulikia changamoto zinazojitokeza lakini aliwahimiza wananchi kuhakikisha wanakuwa na bima ya afya.

Mapema Waziri waAfya, Maendeleo ya  Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alimuambia Makamu wa Rais kuwa (MAMC) Mloganzila ni kati ya hospitali saba zinazomilikiwa naserikalia mbazo zinatoa huduma za matibabu ya kibingwa ngazi ya juu pia alimpongeza Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa kuweka msukumo wake katika  huduma ya mama na motto ambapo juhudi za Makamu wa Rais zimezaa matunda ambapo leo hii kuna vituo 208 vimeboreshwa na kutoa huduma.

Wakati huohuo, Naibu Waziri waElimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Ole Nasha amesema wanafunzi 350 wa shahada ya kwanza wameanza kupata mafunzo ya udaktari na udaktari bingwa na kuishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuona umuhimu wa maendeleo ya upanuzi wa kamapsi hii ili kuruhusu udahili wa wanafunzi wengi.