Kiswahili | English
Site Keyword Search:
    
 
Total site visits: 3115462.
Baraza la wafanyakazi katika Ofisi ya Makamu wa Rais limetakiwa kuwa sehemu sahihi ya kujadili na kutatua migogoro ya wafanyakazi na siyo majukwaa ya siasa.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe January Mkamba, alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli jijini Dar  es Salaam.

Mhe. Makamba alisema kuwa vikao vya baraza la wafanyakazi vimekuwepo kisheria na ni muhimu wajumbe kukaa pamoja kujadili masuala ya msingi yanayowahusu watumishi kwani wao ndio waliowachanga hivyo, majadiliano yanayokuwepo  katika vikao hivyo ni nyenzo muhimu ya kuondoa migogoro na migomo mahala pa kazi.

“Nyie ni miongoni mwa watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais ambao kwa namna moja au nyingine mmeaminiwa na kukabidhiwa dhamana ya kuwawakilisha wenzenu katika chombo hiki muhimu, katika kuamua na kushauri Baraza juu ya masuala mbalimbali yanayolenga kuleta ufanisi na utulivu ndani ya Ofisi yetu, alisisiza Makamba”.

Aidha, Waziri Makamba alisema kwamba, Lengo la vikao vya Baraza ni kuleta ufanisi wa utendaji kazi mahala pa kazi kwa ajili ya manufaa ya Taifa  kuelekezana, kushauriana na kukumbushana, kuhusu majukumu ya ofisi  na ushiriki wa wafanyakazi katika kuyatekeleza na kuyasimamia, na aliongeza kusema kuwa  ni fursa ya kipekee ya kutafakari utendaji wa kazi na majukumu ya Ofisi kwa ujumla.

Kikao hicho cha baraza la wafanyakazi cha Ofisi ya Makamu wa Rais kimehudhuriwa na wawakilishi kutoka TUGHE Taifa na Mkoa na Wawakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Zanzibar.

 

 


 

<< View list of News and Events.