Kiswahili | English
Site Keyword Search:
    
 
Total site visits: 3306236.Listed below are the latest items of news:
MAKAMU WA RAIS AZINDUA MAKUMBUSHO MAPYA YA OLDUVAI

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro, wengine pichani  ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) pamoja na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kulia).

Posted: 5th Oct 17

NAIBU WAZIRI LUGOLA AWASILI OFISI YA MAKAMU WA RAIS

 

Naibu Waziri Mhe. Kangi Lugola  akisalimiana na Mkurugenzi wa Mazingira Bw. Richard Muyungi mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Makamu wa Rais, kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Prof Faustin Kamuzora

Posted: 10th Oct 17

NAIBU WAZIRI MH. KANGI LUGOLA AKILA KIAPO - IKULU

 

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dar es Salaam, kufuatia mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Mhe. Rais hivi karibuni

Posted: 12th Oct 17

NAIBU WAZIRI MH. KANGI LUGOLA AKUTANA NA WATUMISHI WA OFISI YAKE

 

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola akizungumza na sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Dar es Salaam na kuwaasa kufanya kazi kwa bidii, umoja, na kuhakikisha kila mtu anatimiza wajibu wake. Mkutano huo umefanyika Mtaa wa Luthuli Dar es Salaam.

Posted: 17th Oct 17

PROF KAMUZORA NA DKT KUSULUKA WAONGOZA KIKAO KAZI CHA KUJADILI RASIMU YA SERA YA ARDHI

 

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (kushoto) akiwa na Dkt. Moses Kusuluka Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Viongozi hawa pamoja na wataalamu wengine wamekutana katika kikao kazi Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam, kupitia rasimu ya sera ya Ardhi.

Posted: 6th Oct 17

UGENI KUTOKA BENKI YA DUNIA WAMTEMBELEA PROF. KAMUZORA

 

Prof. Faustin Kamuzora (Katikati) Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais mara baada ya kukutana na ugeni kutoka Benki ya Dunia. Watatu kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu Eng. Ngosi Mwihava. Pamoja na mambo mengine ugeni huo uliwasilisha taarifa yao mara baada ya kutembelea Mradi wa Kihansi hivi karibuni.

Posted: 16th Oct 17

WAZIRI MAKAMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA SWEDEN

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (kushoto) akibadilishana mawazo na Balozi wa Sweden Nchini, Katarina Rangnitt (kulia) Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora.

Posted: 12th Oct 17

WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA BALOZI WA NORWAY

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini  Tanzania Hanne-Marie Kaarstad (katikati) Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kuendelea kushirikiana katika sekta ya Hifadhi na Usimamizi endelevu wa mazingira nchini.

Posted: 16th Oct 17

WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA ZANZIBAR

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  Muungano na Mazingira Mhe January Makamba akifafanua jambo mbele ya  kusanyiko la wanajumuiya ya Wafanyabiashara wa Zanzibar. Kikao hicho kimefanyika hii leo eneo la Kinazini Zanzibar. Wengine katika picha ni viongozi wa Jumuiya hiyo.

Posted: 19th Oct 17

WAZIRI MAKAMBA ATEMBELEA OFISI ZA URATIBU - SMZ

 

Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Uratibu - Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri January Makamba mara baada ya kutembea Ofisi zao zilizopo Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam.

Posted: 5th Oct 17

  
 

30th Nov -1